Rais Dkt.Mwinyi amshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuandaa Futari iliyowaleta viongozi na wananchi pamoja

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Februari 19,2026 amejumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali,Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa Siasa, Dini pamoja na wananchi katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika Viwanja vya Ikulu ndogo ya Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
"Ninamshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kuandaa futari hii iliyotukutanisha pamoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
"Tukio hili limeendelea kuimarisha mshikamano, umoja na ushirikiano baina ya viongozi na wananchi, pamoja na kuonesha dhamira ya pamoja ya kuendeleza amani na maendeleo ya Taifa letu.Ramadhani ni mwezi wa ibada, huruma na kujenga mahusiano mema.
"Tuendelee kushikamana, kuheshimiana na kushirikiana kwa manufaa ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla,"ameeleza Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here