SINGIDA-Wananchi wa Kata ya Unyamikumbi, Singida wamehimizwa kuhakikisha wanamiliki ardhi kisheria na kuweka alama za kudumu za mipaka ili kuepusha migogoro ya ardhi.
Akitoa elimu hiyo, Mkaguzi wa Polisi Kata ya Unyamikumbi, Inspekta Saidi January amesisitiza matumizi ya njia sahihi za usuluhishi pale migogoro inapotokea na umuhimu wa kuhudhuria elimu ya sheria mara kwa mara.Pia,amekemea vikali tabia ya kuuza eneo moja kwa watu zaidi ya mmoja, akieleza kuwa ni kinyume cha sheria na chanzo cha migogoro katika jamii.
Wananchi wamekumbushwa kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati ili kulinda amani ya maeneo yao.
