NA DIRAMAKINI
MSHAMBULIAJI wa Young Africans ya Dar es Salaam, Laurindo Dilson (Depu) amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, huku Steve Barker wa Simba akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 16,2026 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
Laurindo alionesha kiwango kizuri chenye mwendelzo kwa mwezi huo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili katika michezo miwili ambayo Young Africans ilicheza na kuisaidia timu yake kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Mshambuliaji huyo aliwashinda beki Rushine De Reuck wa Simba na kiungo Idd Selemani ‘Nado’ wa Azam alioingiana fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa upande wa Barker aliyeingia fainali na Pedro Goncalves wa Young Africans na Florent Ibenge wa Azam alioongoza timu yake kushinda michezo miwili na kutoka sare mmoja hivyo kupanda kutoka nafasi ya sita hadi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Wakati huo huo Meneja wa Uwanja wa Isamuhyo, Said Mpuche, amechaguliwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Februari kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.
Katika hatua nyingine Ramadhan Karanje wa B19 amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Februari wa Ligi ya NBC Championship 2025/26, huku Mbwana Makata wa Polisi Tanzania akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi huo.
Karanje aliyeingia fainali na Obrey Chirwa wa Kagera Sugar na Tariq Seif wa Polisi Tanzania, alionesha kiwango chenye mwendelzo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne (4) kwa dakika 404 za michezo mitano aliyoicheza.
Kwa upande wa Makata aliyeingia fainali na Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Zuberi Katwila wa Geita Gold, aliiwezesha timu yake kushinda michezo minne na kutoka sare mmoja hivyo kupanda kutoka nafasi ya sita hadi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ya NBC Championship.
MABAO BORA ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
1. Mathew Tegisi (89') - Pamba vs Coastal Union
2. Shekhan Ibrahim (89') - Yanga vs JKT Tanzania
3. Ismail Mhesa (86') - Mtibwa vs Tanzania Prisons
2. Shekhan Ibrahim (89') - Yanga vs JKT Tanzania
3. Ismail Mhesa (86') - Mtibwa vs Tanzania Prisons
Tags
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
Habari
Kocha Bora wa Mwezi
Laurindo Dilson
Ligi Kuu ya NBC
Michezo
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi
