Magazeti leo Machi 27,2026

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetoa onyo la mwisho kwa taasisi zote zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi kujisajili kabla ya Aprili 8, 2026 ikibainisha kuwa hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa kuanzia Aprili 9,mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 26, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Emmanuel Lameck Mkilia amesema serikali imetoa muda wa kutosha tangu mwaka 2024 kwa taasisi kujisajili ikiwa ni pamoja na kuongeza muda huo mara mbili.

Amesema kuanzia Aprili 9, utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 utaanza rasmi, na taasisi au mtu yeyote atakayebainika kutokujisajili atachukuliwa hatua za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here