MBEYA-Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Anthony Mkwawa amewataka wakazi wa Mkoa wa Mbeya kushirikiana na Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Eid el Fitri.
Rai hiyo ameitoa Machi 19, 2026 kupitia redio Dream Fm ya jijini Mbeya ambapo ameikumbusha jamii suala la umuhimu wa utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali ili kutanzua uhalifu kwa wakati.
Rai hiyo ameitoa Machi 19, 2026 kupitia redio Dream Fm ya jijini Mbeya ambapo ameikumbusha jamii suala la umuhimu wa utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali ili kutanzua uhalifu kwa wakati.Aidha, amewataka kuchukua tahadhari zote za kiusalama hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na mvua zinazoendelea kunyeesha katika maeneo mbalimbali.
Naye, Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilomba ambaye pia ni Polisi Kata ya Ilomba Mkaguzi wa Polisi Athuman Kimeza ametoa wito kwa wazazi na walezi kuzingatia ulinzi wa Mtoto katika kipindi hiki cha Sikukuuu ikiwa ni pamoja na Haki na wajibu wa mtoto kwa mujibu wa Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009.
Pia, amesisitiza umuhimu wa kuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi katika kulinda makazi yao na maeneo mbalimbali ili kuzima mianya ya uhalifu na wahalifu.