Mwanasheria Mkuu wa Serikali aungana na viongozi mbalimbali kuaga mwili wa Waziri Lukuvi jijini Dodoma

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza S. Johari ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi.
Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, leo Machi 27, 2026.
Aidha,misa ya kuaga mwili imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mwigulu Lameck, ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa walihudhuria kutoa heshima zao za mwisho.
Mheshimiwa Lukuvi alifariki dunia Machi 25,2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here