Naibu Waziri wa Fedha akutana na Kampuni ya PLASCO kujadili maendeleo ya viwanda

DAR-Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), kwaniaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya PLASCO inayojihusisha na uzalishaji wa mabomba ya plastiki yanayotumika katika miundombinu ya maji na gesi, ukiongozwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Dario Manlubatan, akiambatana na Meneja wake wa Masoko, Bi. Edith James, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili mchango wa sekta ya viwanda katika kukuza uchumi wa nchi.
Mhe. Luswetula aliahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi, kushughulikia changamoto zao, pamoja na kuendelea kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara na uwekezaji ili kukuza maendeleo ya uchumi wa nchi.
Kwa upande wa Kampuni ya Plasco, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Dario Manlubatan, alieleza utayari wao wa kushirikiana na Serikali katika miradi ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na kuleta ubunifu na utaalamu utakaosaidia kuimarisha miundombinu ya miradi ya maji na kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here