DODOMA-Leo Machi 31,2026 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mheshimiwa Profesa Riziki Shemdoe, amewasilisha rasimu ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Mheshimiwa Profesa Shemdoe amewasilisha rasimu hiyo inayojumuisha mafungu 37 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye anatarajiwa kuwasilisha rasmi makadirio hayo kesho, Aprili 1, 2026 katika kikao cha pili cha mkutano wa tatu wa Bunge la Bajeti.
Katika kikao hicho,wabunge watapata fursa ya kujadili kwa kina mipango, vipaumbele pamoja na matumizi ya fedha yaliyopangwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka husika wa fedha, kabla ya kupitishwa kwa bajeti hiyo.
