ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Baraza la Eid el-Fitri litakalofanyika siku ya Jumamosi, tarehe 21 Machi 2026, kuanzia saa 3:45 asubuhi, katika Ukumbi wa Polisi Ziwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
