DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amewahimiza watanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano wa kitaifa ili nchi iendelee kupata utulivu na kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
Mhe. Balozi Omar ametoa wito huo wakati akifungua mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya AL Khairiyya Islamic Foundation, yaliyofanyika katika Viwanja vya Kibada Garden, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Ametokea mfano wa vita vinavyoendelea Mashari ya Kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran namna vilivyo athiri makundi mbalimbali ya kijamii vikiwemo vifo vya idadi kubwa ya watu.
Aidha, Mhe. Balozi Omar, alielezea umuhimu wa jamii hususan vijana wa Kiislam kushika maadili mema kwa kuhifadhi maneno ya Mwenyezi Mungu mioyoni mwao na kuyaishi katika tabia zao.






