Viongozi wa Hale AMCOS mahakamani kwa rushwa na uhujumu uchumi Tanga

TANGA-Leo Machi 25,2026 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Tanga imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 5540/2026 mbele ya Mheshimiwa Mwajombe, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga dhidi ya Bw. Julius Msafiri Ngome ambaye ni Mhasibu wa Hale AMCOS.
Wengine ni Bw. Mawala Samwel Barnaba ambaye ni Meneja wa Hale AMCOS, Bi. Irene Joseph Mbezi ambaye ni Mhudumu wa ofisi na Bi. Rhoda George Chomola ambaye ni mke wa Bw. Mawala Samwel Barnaba, Meneja wa Hale AMCOS.

Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa mawili ya kujipatia manufaa kinyume na kifungu cha 23(1)(b) na Matumizi Mabaya ya Mamlaka kinyume cha kifungu cha 31, vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 R.E 2022.

Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU,Bi. Khadija Luwongo amesema,kati ya Januari Mosi,2022 na Desemba 31,2022 katika eneo la Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga Bw. Julius Msafiri Ngome na Mawala Samwel Barnaba wakiwa katika utekelezaji wa majumu yao, walitumia vibaya madaraka yao kwa kufanya malipo yasiyo halali ya kiasi cha shilingi 6,956,936.00.

Ni kwa Bi. Rhoda George Chomola na kiasi cha shilingi 5,039,900.00 kwa Bi. Irene Joseph Mbezi kwa madai kwamba waliwasilisha mkonge Hale AMCOS, jambo ambalo si kweli.

Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni na Sheria ndogo za Hale AMCOS na kimepelelekea walipwaji kupata manufaa ambayo hawakustaili kwa mujibu wa sheria. Washtakiwa walikana makosa yote yanayowakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here