Wachimbaji wadogo Mbogwe washauriwa kufuata kanuni za msaada wa kiufundi

GEITA-Wachimbaji wadogo wa madini Mkoa wa kimadini Mbogwe wametakiwa kuzingatia Kanuni za Msaada wa Kiufundi zilizotangazwa na Serikali ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuepuka migogoro isiyo ya lazima na wawekezaji.
Rai hiyo ilitolewa Machi 13, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wakati wa ziara yake ya kikazi katika mgodi wa Peter Kisura Kawe na Washirika uliopo wilayani Mbogwe.

Dkt. Kiruswa alisema kuwa ni vyema kuzingatia Kanuni mpya za mwaka 2025 zinazoratibu ushiriki wa watoa msaada wa kiufundi katika leseni ndogo za uchimbaji.

Dkt.Kiruswa alieleza kuwa, mikataba yote ya msaada wa kiufundi kati ya mchimbaji mdogo na mtoa huduma lazima isajiliwe rasmi Tume ya Madini.

Dkt.Kiruswa alifafanua kuwa, kanuni zinaelekeza kuwepo kwa uwazi katika mgawanyo wa mapato ya madini yatakayozalishwa ili kumlinda mchimbaji mdogo.

Aliongeza kuwa, msaada wa kiufundi unapaswa kulenga kuongeza ujuzi, kutoa teknolojia ya kisasa, na kuongeza kiasi cha madini kinachopatikana.
Dkt.Kiruswa alisisitiza kuwa,wachimbaji wadogo wana fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia programu maalum za kibenki kama CRDB Bank zilizozinduliwa hivi karibuni.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa kimadini Mbogwe Mhandisi Ludovick Mwacha alisema mpaka sasa mkoa wa kimadini Mbogwe umefikia asilimia 75.81 makusanyo ya lengo la Mwaka 2025/2026.

Awali, akitoa taarifa ya mwenendo wa uzalishaji katika mgodi wa Peter Kisura na Washirika, Meneja Mgodi Mhandisi Samson Mathias alisema, mgodi ulianza uzalishaji rasmi mwaka 2025 na mpaka sasa unazalisha kilogramu nane kwa mwezi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here