Dkt.Edward Hossea ampongeza Rais Dkt.Samia kwa kuunda Tume ya Uchunguzi

IRINGA-Rais mstaafu wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS),Dkt.Edward Hosea amepongeza hatua ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuunda Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Kabla na Baada ya Oktoba 29,2025.
Dkt.Hossea amesema hayo mkoani Iringa mapema leo wakati akizungumza na wanahabari na kueleza kuwa uwepo wa tume hiyo kumesaidia kufanya watanzania, kutulia na kusubiri mapendekezo ya tume yatalenga nini hasa na kusisitiza watanzania wana matumaini na tume hii.

“Ninapongeza hatua ya Mheshimiwa Rais ya kuunda tume,fikiria tusingekuwa na tume hali ingekuwaje?Kuwepo kwa tume hii kumesaidia kuwafanya watanzania watulizane wawe na matarajio kuona tume hii inapendekeza nini,kwa hivyo mimi nimaamini kabisa tume hii watanzania wana matumaini makubwa sana,”amesema Dkt.Hossea.

Dkt.Hossea ameongeza kuwa,pamoja na yote yaliyotokea ataendelea kuwa muumini wa Tanzania kutafuta suluhu zake yenyewe hata kama taasisi za kimataifa zitakuja Tanzania na kutaka kujua kilichotokea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here