Kamati Elekezi ya Taifa ya Huduma Jumuishi za Fedha yakutana Dar kujadili upatikanaji wa huduma za fedha nchini

DAR-Kamati Elekezi ya Taifa ya Huduma Jumuishi za Fedha, ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, imekutana jijini Dar es Salaam tarehe 23 Aprili 2026 kujadili mikakati ya kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma za fedha nchini.Katika kikao hicho, wajumbe walijadili kwa kina juhudi zinazoendelea kufanywa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kuimarisha ujumuishaji wa kifedha.
Miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele ni utoaji wa elimu ya fedha kwa makundi tofauti ya jamii, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa programu ya utoaji ithibati kwa watoa elimu ya fedha, inayoratibiwa na Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania.

Kamati ilibaini umuhimu wa kuendelea kuimarisha elimu ya fedha kwa wananchi ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika huduma rasmi za kifedha.

Elimu hiyo inalenga kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya huduma za fedha, hatua itakayochangia kuboresha ustawi wa kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Kamati Elekezi ya Taifa ya Huduma Jumuishi za Fedha inaundwa na wanachama 33 katika ngazi ya wakurugenzi na makamishna, wanaotoka katika wizara na taasisi mbalimbali za Serikali, mamlaka za udhibiti, pamoja na vyama vinavyohusika na sekta ya huduma za fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here