Wizara ya Maji kwa kushirikiana na taasisi binafsi imeandaa mafunzo kuhusu usalama wa mabwawa Ili kuhakikisha mabwawa yanaendelea kuwa salama kwa matumizi yaliyokusudiwa hapa nchini.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Wizara ya Maji Bw. Robet Sunday akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano Wizara ya Maji Mtumba jijini Dodoma ametaja taasisi zinazoshirikiana na Wizara ya Maji kuwa ni Chemba ya Migodi Tanzania (CMT) na Kampuni ya Uhandisi ya City.
Mafunzo hayo yanatarajia kufanyika jijini Mwanza kuanzia Oktoba 21 hadi 23, 2026 yakilenga kuendelea kutoa elimu kwa wadau na wataalamu wa mabwawa ili kuhakikisha usanifu, ujenzi na uendelezaji wa mabwawa ya maji na mabwawa ya tope sumu yana viwango ili kulinda mazingira na vyanzo vya maji.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























