Magazeti leo Aprili 7,2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nchini na vijana kuendelea kulinda na kutetea misingi ya Muungano iliyoachwa na Waasisi.
Mhe. Mhandisi Masauni ameyasema hayo Aprili 06, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano maalum la kumuenzi aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Waziri Masauni amesema mwasisi huyo wa Muungano ameacha alama na historia ya kudumu kwa vizazi vya sasa na vijavyo, juhudi zilizotokana na mchango alioutoa katika kuwaunganisha Watanzania na kupambania maslahi ya wananchi wanyonge.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here