DAR-Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Olympic Committee (TOC), Rahim Kalyango, amelalamikia kuvunjwa kwa kanuni za uchaguzi pamoja na kukiukwa kwa baadhi ya vifungu vya kisheria vinavyoongoza mchakato wa uchaguzi wa kamati hiyo.
Akizungumza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kalyango alisema kuwa kuna taratibu muhimu ambazo hazikufuatwa ipasavyo katika maandalizi ya uchaguzi huo, na hivyo kuhatarisha uhalali na uwazi wa mchakato mzima.
Kutokana na hilo, ameomba serikali kuingilia kati na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia sheria, misingi ya haki, na usawa kwa wagombea wote.
