ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa mkono wa pole kwa wanafamilia wa marehemu Mahmoud Muhammed Mussa, aliyekuwa Mstahiki Meya Mstaafu wa Jiji la Zanzibar, aliyefariki jana.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa pole tarehe 07 Machi 2026, alipofika nyumbani kwa marehemu Pangawe, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj Dkt. Mwinyi amewanasihi wanafamilia kuwa na subira kipindi hiki cha msiba mzito wa kuondokewa na mpendwa wao.
Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa anatarajiwa kuzikwa leo tarehe 07 Aprili 2026, kijijini kwao Shakani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)