ZANZIBAR-Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Aprili 7, 2026, amehani msiba na kutoa pole kwa Mheshimiwa Tunu Kondo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Zanzibar na Mbunge wa Viti Maalum, kufuatia kifo cha Mstahiki Meya Mstaafu wa Jiji la Zanzibar, Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa, alipofika nyumbani kwa marehemu Zanzibar.
Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa alifariki dunia Aprili 6, 2026. Wakati wa uhai wake, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali, ikiwemo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi (BLW).





