DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn, katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Mei 2026, katika kikao chenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kifedha kati ya nchi hizo mbili.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa karibu katika sekta za fedha ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja za kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi wa Tanzania.


