Magazeti leo Juni 3,2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za Dini nchini kuimarisha maadili kwa jamii na kukuza maemdeleo.
Mhe. Sangu amesema hayo alipomwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika hafla ya kumsimika uaskofu mchungaji Daniely Liyaseke wa Kanisa la The Charismatic Episcopal Church of Tanzania, Dayosisi mpya ya Ukanda wa Tanzanite One, iliyofanyika Mei 31, 2026 Kijiji cha Terat, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Sangu amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa makanisa katika kuimarisha maadili, mshikamano wa kijamii na maendeleo ya Taifa na itaendeleza ushirikiano huo. Ameongeza kuwa kauli mbiu ya kanisa hilo “Kwa neema ya Mungu, tunajenga Huduma kwa vizazi vya sasa na vijavyo” inaakisi dhamira ya kuwekeza kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here