DODOMA-Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaungana na Mashirika mengine ya Umma, kushiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park, Dodoma kuanzia Juni 16 hadi 23, 2026.
Kupitia maadhimisho haya yenye kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu,” TRC inaendelea kuonesha dhamira yake ya kutoa huduma bora, salama na endelevu za usafiri wa reli, huku ikiwa karibu zaidi na wananchi kwa kutoa elimu kuhusu huduma zake, miradi ya mbalimbali ya ujenzi wa reli na mchango wa sekta ndogo ya reli katika kukuza uchumi wa Taifa.
TRC inakukaribisha ewe mwananchi katika banda lake usikie bidhaa na huduma ilizoleta katika WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026!.




