Waziri wa Mambo ya Nje wa Slovakia kufanya ziara ya kikazi Tanzania tarehe 10 hadi 11 Juni, 2026

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya wa Jamhuri ya Slovakia, Mhe. Juraj Blanár, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Juni 10 na 11, 2026.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Slovakia.

Akiwa nchini, Mhe. Blanár atafanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt.Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), yatakayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za utalii, elimu, programu za ufadhili wa masomo, usalama wa mtandao, biashara na uwekezaji.

Mhe. Blanár akiambatana na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Dkt. Kombo (Mb.), watashiriki katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Slovakia jijini Dar es Salaam, ambao uliofunguliwa mwezi Novemba 2025.

Uzinduzi wa Ubalozi huo unaakisi dhamira ya pamoja ya Tanzania na Slovakia ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua maeneo ya ushirikiano.

Mhe. Blanár pia atashiriki katika Kongamano la Biashara la Tanzania Slovakia ambalo litawakutanisha viongozi wa biashara na wawakilishi wa sekta binafsi kutoka nchi zote mbili kwa lengo la kuangalia fursa za biashara na uwekezaji, kukuza uhamishaji wa teknolojia, na kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati zikiwemo nishati jadidifu, uchakataji wa mazao ya kilimo na ubunifu wa kidijitali.

Kwa ujumla, ziara hiyo inatoa fursa muhimu ya kuendeleza ushirikiano wa pande mbili, kupanua maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Slovakia.

Aidha, inatarajia kutoa msukumo mpya katika uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Slovakia, ambayo yana mizizi tangu enzi za iliyokuwa Czechoslovakia.

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii kutoka Slovakia
wanaotembelea Tanzania na hivyo kufungua fursa mpya za ushirikiano katika sekta ya utalii na kuimarisha uhusiano wa watu kwa watu kati ya Tanzania na Slovakia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here