Rais Dkt.Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 22,2026 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na uhamisho huo ni kama ifuatavyo:

(i) Dkt. Latifa Mohammed Khamis ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Khamis alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE);

(ii) Bi. Prisca Burton Lwangili ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menegmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Lwangili alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI;

(iii) Bw. Abdallah Hassan Mitawi amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi;

(iv) Balozi Baraka Haran Luvanda amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria;

(v) Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi;

(vi) Dkt. Maduhu Isaac Kazi amehamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Mazingira; na

(vii) Bw. Ephraim Balozi Mafuru ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mafuru alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Aidha, uapisho wa Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here