BoT kuzindua kielelezo cha faida rejea ya dhamana za serikali (Tanzania Sovereign Yield Curve)

NA DIRAMAKINI

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuzindua rasmi kielelezo cha faida rejea ya dhamana za serikali (Tanzania Sovereign Yield Curve).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma Agosti 5,2026, BoT imeeleza kuwa, uzinduzi huo umepangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya Agosti 7,2026 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.

"Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza soko la ndani la dhamana za Serikali, ikitarajiwa kuleta uwazi sokoni, kuboresha upatikanaji wa bei halisi za soko, kuchochea ukuaji wa soko la upili na kuweka msingi thabiti na wa kuaminika katika kupanga bei za dhamana za Serikali pamoja na bidhaa nyingine za kifedha."

Aidha,Benki Kuu ya Tanzania imewakaribisha wadau mbalimbali wa sekta ya fedha wakiwemo watoa elimu ya fedha pamoja na wawekezaji wote kushiriki katika uzinduzi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here