Kadama English Medium yaongoza Kanda ya Ziwa mtihani wa TAPIE

GEITA-Shule ya Msingi ya Kadama English Medium imechukua nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba wa Kanda ya Ziwa ulioandaliwa na Umoja wa Wamiliki wa Shule Binafsi Kanda ya Ziwa kupitia Tanzania Association of Private Investors in Education (TAPIE).
Katika matokeo hayo Kadama English Medium imepata wastani wa alama 47.7 ambao ni ambalo ni daraja A.Wanafunzi wote wa shule hiyo waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kupata wastani wa Daraja A.

Ushindi huo umeifanya shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 17 zilizoshiriki katika mtihani huo wa pamoja wa Kanda ya Ziwa.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Shule ya Waja Spring huku Peace Land Primary School ikishika nafasi ya tatu.
Mkurugenzi wa Kadama English Medium, Leticia Pastory amesema,shule hiyo itaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha inatoa elimu bora pamoja na maandalizi mazuri ya wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya kitaifa.

Aidha,amewataka wazazi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa shule hiyo ili iweze kuendeleza tunu yake ya kuwapatia wanafunzi elimu bora pamoja na malezi yanayozingatia maadili mema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here