Miili ya askari polisi waliofariki baada ya kugongwa na gari Kibaha yaagwa leo

PWANI-Miili ya askari wawili wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani waliofariki Agosti 25, 2026 baada ya kugongwa na gari eneo la kivuko cha watembea kwa miguu (zebra) eneo la Maili Moja imeagwa leo na kusafirishwa kwenda mikoani kwao kwa maziko.
Tukio la kuaga miili ya askari hao wa Jeshi la Polisi Kostebo Izdory George Michael na askari wa kike Rehema Juma Magawa limeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, ambapo askari wa vyeo mbalimbali na waombolezaji wengine wameshiriki katika kuaga.
Mwili wa Marehemu Rehema umesafirishwa kwenda Korogwe Mkoani Tanga kwa mazishi na Mwili wa Izdory umepelekwa Mkoa wa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini kwa mazishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here