Mtoto aokotwa Igawa wilayani Mbarari, saidia wapatikane wazazi au ndugu zake

NA DIRAMAKINI

MTOTO anayejitambulisha kwa jina moja la Side ameokotwa katika eneo la Igawa wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, huku jitihada zikifanyika kuwapata wazazi au ndugu zake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na watu waliompokea mtoto huyo, Side anasema anatoka Mbeya, lakini hawezi kutaja eneo au sehemu anayotoka.

Pia, mtoto huyo hajui majina ya wazazi wake; anasema baba yake anaitwa Side na mama yake pia anaitwa Side.

Aidha, mtoto huyo ameeleza kuwa hasomi, jambo linaloweza kufanya utambuzi wa familia yake kuwa mgumu zaidi.

Kwa sasa mtoto huyo yupo chini ya uangalizi wa Mwenyekiti wa Kitongoji ambaye anaendelea kusaidia katika jitihada za kuwatafuta wazazi au ndugu zake.

Wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia kumpata mzazi, ndugu au mtu anayemfahamu mtoto huyo wanaombwa kutoa taarifa kwa wahusika kupitia namba zifuatazo:

Mwenyekiti wa Kitongoji: 0763 775 034

Mwalimu Mkuu, Shule ya Msingi Igomelo: 0756 805 049

Tafadhali sambaza taarifa hii katika makundi ya WhatsApp, mitandao ya kijamii na kwa wananchi wengine ili kuwafikia wazazi au ndugu wa mtoto huyu.

Mtu mwenye taarifa sahihi anashauriwa kuwasiliana na wahusika waliotajwa hapo juu au mamlaka husika za eneo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here