Tuungane kuhubiri amani katika jamii yetu-SACP Malulu

DAR-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP Kungu John Malulu Agosti 3,2026 amefanya mazungumzo na Katibu wa Viongozi wa Amani wa wilaya ya Temeke Mchungaji Titus Kiyame.
Kamanda Malulu amesema, lipo jukumu kubwa la kulinda na kuimarisha amani kwa nguvu kubwa katika makundi yote ndani ya jamii na Jeshi la Polisi linafanya hivyo, lakini viongozi wa dini wana jukumu kubwa.

Aidha, Mkuu wa Polisi Jamii wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Emma Foya amemwambia Mchungaji kuwa katika Kitengo cha Polisi Jamii ipo miradi mingi ambayo kimsingi ni madarasa ya uponyaji na ualimu juu ya umuhimu wa kuilinda na kuitetea kwa nguvu kubwa amani iliyopo.

Naye Mchungaji Titus ambaye ni Katibu wa Viongozi wa Amani Temeke ameshukuru kwa kikao hiko kizuri kilicholenga kuboresha zaidi ushirikiano baina yao na ameahidi yote waliyoyazungumza watayafanyia kazi ili Temeke na nchi nzima kwa ujumla amani itamalaki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here