NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na kumpangia kituo Balozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 6,2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka, uteuzi na kupangiwa kituo ni kama ifuatavyo:
(i) Dkt. Suleiman Peter Kiula ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).Dkt.Kiula anachukua nafasi ya Bw.Shaibu Ramadhan Matessa ambaye atapangiwa majukumu mengine; na
(ii) Balozi Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia.
