NJOMBE-Wananchi kata ya Matola Wilaya ya Njombe wamehimizwa kuimarisha ushirikiano katika kutunza na kulinda amani, usalama na umoja kwenye maeneo yao kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwenye vyombo vya dola ili kudhibiti matukio hayo yanayorudisha nyuma maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Polisi kata hiyo, Mkaguzi wa Polisi INSP Happyrose Haule wakati akitoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Mbega katika kata hiyo ambapo ameeleza kuwa ulinzi wa amani ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo katika jamii.
Aidha,amewahimiza kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo katika ngazi ya kijiji ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuwezesha kuwabaini wahalifu mapema kabla hawajatekeleza vitendo hivyo.
Utoaji wa elimu ya ushirikishaji jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu unaenda sambamba na maandalizi kuelekea maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi jamii ambayo yanaambatana na kaulimbiu ya "MIAKA 20 YA POLISI JAMII; TUSHIRIKIANE KUIMARISHA AMANI, USALAMA NA UMOJA WA KITAIFA".
