Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo Agosti 26, 2022

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 26, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo unaanza leo Agosti 26, 2022.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Mtumwa Iddi Hamad kywa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Kabla ya uteuzi huo, Mtumwa alikuwa Afisa Utumishi na Uendeshaji katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar.

Pili, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua,Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya uteuzi ho, Ulfat alikuwa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Abdulrahman AL-SUMAIT Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments